Uzinduzi wa BBA 2013 'THE CHASE' kwa Tanzania ulifanyika katika ndani ya kiota cha Samaki Samaki jijini Dar es Salaam huku wageni mbali mbali waliweza kujipatia vinywaji na chakula cha kutosha. Hakika uzinduzi huo ulifana sana kwa vile watu wengi wametokea kuwapenda washiriki na waliweza kuwazungumzia vizuri, tuzidi kumwomba Mungu awasimamie washiriki wetu na waweze kufanya vyema.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akitoa mwongozo wa shughuli za uzinduzi kabla ya kuanza kwa Show ya Big Brother The Chase 2013 Kiota cha Maraha cha Samaki Samaki kilichopo maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam.
 Kabla ya kuanza uzinduzi wa Show ya Big Brother The Chase 2013 dennis fusi daily news/habari leo ilichezeshwa bahati nasibu ndogo iliyompelekea mdau huyu (kushoto) kuibuka na Tablat mpya kabisa.kulia ni Mshereheshaji wa hafla hiyo,Millard Ayo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini, mbwene Yessaya a.k.a AY akisoma kikaratasi wakati akimtaja mshindi wa bahati nasibu ya shilingi laki moja.
Pongezi kwa mshindi wa kitita cha sh. laki moja.
bahati nasibu ikiendelea.
Wadau sie tukiwakilisha ndani ya Samaki Samaki, toka shoto ni Missie Populer, Othman Michuzi, B12, Jimmy, Mdau pamoja na Cathbert Angelo 'Kajunason Blog'.
Wakilishi wa Airtel Tanzania, Dangio na Jannet.
Mwandishi wa Habari wa TBC1, Njedengwa akitafakari jambo.
Kila mmoja alikuwa na furaha.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi na akiteta jambo na mshereheshaji wa shughuli hiyo, Millard Ayo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko DStV, Furaha Samalu akiwa na Mkurugenzi wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe.
Bahati nasibu ya kufungua box lenye zawadi huku kila mmoja akiwa na funguo yake.
Mmiliki wa Blog hii, Cathbert Angelo nae alipata fursa ya kumchagua mshindi wa bahati nasibu toka katika kuchagua jina toka kwenye kindoo ambapo Asha Baraka alifanikiwa kuwa mshindi na kujipatia kitita cha shilingi laki moja.
Ni shangwe kwa kwenda mbele pale Mtanzania Feza Kessy alipoonekana ndani ya Jumba la Big Brother.
Wadau wakishoo lavu ndani ya Samaki Samaki.
Wengi walikuwa wakifuatilia kwa umakini zoezi hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: